IGP Sirro leo aanika Mbinu za Kumaliza Mauaji Kibiti

Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro ametuma salamu kwa  kikundi cha uhalifu wa mauaji ya baadhi ya askari, raia na viongozi wa wilaya za Kibiti, Jaribu,  na Rufiji katika Mkoa wa Pwani. Kwa kusema kuwa jeshi hilo halitachukua muda mrefu kulipa ubaya wao kwa mujibu wa sheria, kulingana na mauaji waliyofanya.
IGP Sirro ametoa salamu hizo leo Mei 31, 2017, wakati akizungumzia mikatati yake ya kutokomeza mauaji hayo, ambapo ametangaza dau la shilingi milioni 10 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa sahihi zitakazosaidia jeshi hilo kukamata wahalifu hao.
“RPC Pwani alishatoa ahadi yake kwamba atakayetoa taarifa za uhakika kutusaidia kukamata watuhumiwa aliowataja atatoa milioni 5, mimi IGP natoa Milioni 10 kama kuna taarifa yoyote basi watupe taarifa. Majibu ya Pwani hayatachukua muda mrefu,” amesema na kuongeza.
“Na ningependa vitendo vizungumzwe zaidi ya maneo, tatizo la mkoa huo kuna kikundi cha watu wachache wanafikiri  wanaweza kuufanya mkoa huo usiwe na amani, niwambie siku zote haki lazima itatoa majibu na niwahakikishie suala hili litakwisha ndani ya muda mfupi. Tupeleke salamu kwamba ubaya huu tutajibu kwa ubaya kwa muijibu wa sheria.”
Ameeleza kuwa, Jeshi hilo linapanga kukutana na wananchi wa maeneo hayo hivi karibuni ili kuzungumza nao juu ya matukio yaliyotokea kwa lengo la kupata ushirikiano wao, na kuwatoa hofu kwamba nguvu inayotumiwa na jeshi hilo sasa ni za mpito katika kuhakikisha linarudisha amani, na kuwataka raia wema kutokimbia makazi yao.
“Kama kuna nguvu ilikuwa inapita kiasi tutajua namna ya kufanya, tusipofanya kazi pamoja  na wananchi kazi itakua ngumu, tutapita kuzungumza na waananchi hasa raia wema,  kipindi hiki ni cha muda, ni suala la muda. Na kama kuna raia aliyeonewa na polisi atoe taarifa. Raia wema wasikimbie,” amesema.
Ameongeza kuwa “Haya mauaji yaliyotokea kwa askari polisi wetu ni ajali kazini, unapopambana na jambazi kuna mawili ufe au uue, ni ajali kazini, inapotokea huonyesha kwa nini imetokea na kwetu ni fursa ya kujipanga ,  wahalifu hao wamekamatwa sana na wanaendelea kukamatwa, hawajatuzidi nguvu na hawatatuzidi nguvu.”
Na Regina Mkonde


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com