Habari ya kusikitisha: Baba na Mama watuhumiwa kumchinja mtoto wao

Jeshi la polisi mkoa wa kaskazini Pemba linaendelea kuwashikilia watu watatu wanaotuhumiwa kuhusika na kitendo cha mauwaji ya mtoto mchanga kwa kutumia kitu chenye makali.

Akizungumza na mwandishi wetu kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini pemba Ali Haji amewataja wanaotuhumiwa na tukio hilo kuwa ni Riziki Juma Makame, Khamis Hamad Ali na Chumu Matari.

Kamanda Haji amesema tukio hilo limetokea juzi saa mbili usiku wa kuamkia siku ya ijumaa katika msitu wa mjini Wingwi

Ameeleza kwamba jeshi la polisi lilipata taarifa hizo kutoka kwa raia wema na ndipo walipochukua hatua za kijeshi nakufanikiwa kuwatia mikononi watuhumiwa hao.

“Tunaendelea kuwahoji watuhumiwa, ambao ni baba wa mtotomama pamoja na bibi wa mtoto”amesema kamanda Haji

Licha ya watuhumiwa wakike kushindwa kuzungumzia tukio hilo lakini baba anayetuhumiwa kuhusika amekiri na kusema kuwa yeye ametumwa na mama mkwe wake amtupe mtoto huyo na sio kuuliwa.

Akizidi kuelezea mkasa huo amesema kua yeye hakusika na kitendo cha kuuwa na kwasababu hakushirikishwa hata kidogo katika mpango huo na kwamba angeshirikishwa asingekubali kufanya hivyo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya micheweni Abedi Juma Ali ameelezea kusikitishwa na tukio hilo na kuviomba vyombo vya sheria kuchukua hatua kali kwa watakao bainika kuhusika na tukio hilo.

Amesema serikali ya wilaya pamoja na vyombo vyake vya ulinzi vitaendelea kushirikiana na wananchi katika kusimamia haki za watoto ili zisikiukwe .

Naye afisa ustawi wa jamiii wilaya hiyo Hamadi Othmani amesema pamoja na elimu inayotolewa na ofisi yake lakini bado baadhi ya wananchi wanaipokea kwa mtizamo tofauti.

Hili ni tukio la kwanza kutokea katika wilaya ya micheweni ya mtoto kuzawaliwa na kuuliwa kwa kutenganishwa kichwa na kiwiliwili na kisha kutupwa msituni.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com