Habari Mpya kutoka kwa Meya wa Jiji la Dar Es Salaam

NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita , jana amezindua mashindano ya ngumi ya kombe la mstahiki Meya na kusisitiza kuwa kuna kila sababu ya kutoa kipaumbele kwenye mchezo huo ili uweze kuwa ajira sambamba na kuibua vipaji kwa vijana.

 Meya Mwita alisema kuwa michezo ni afya na kwamba atajitoa kadiri ya uwezo wake ili kufanikisha mchezo huo kuwa chanzo cha ajira kama ilivyokuwa kwenye nchi za nje.

Alifafanua kuwa nchi nyingine wapo watu walioajiriwa kupitia mchezo huo na kwamba hata hapa kwetu uwezo huo upo lakini kinachotakiwa ni kujitoa na kuthamiria kuwekeza nguvu kubwa kwenye mchezo huo.

“ Mchezo ni afya, leo hii nimefarijika sana kuona vijana wengi waliojitokeza kushiriki mpambano huu, kutokana na hilo kama meya wa jiji hili, na mdhamini mkuu wa mashindao haya, nitakuwa pamoja na nyinyi” alisema Meya Mwita.

Akizungumzia changamoto zilizotolewa na Mwenyekiti wa chama cha ngumi mkoa wa Dar es Salaam, Carol Godfrey ,  Meya mwita alisema  atasaidia kutoa vifaa vya michezo huku changamoto ya uwanja akiahidi kulishughulikia.

Aliongeza kwamba kwakuwa anahitaji maendeleo ya mchezo wa ngumi, atahakikisha kuwa kwa nafasi aliyokuwa nayo anawawezesha wachezaji ikiwa ni lengo la kuhamasisha vijana wengi wenye vipaji vya mchezo huo kujitokeza.

“ Najua wapo vijana ambao wanavipaji wa mchezo huu, lakini bila kuwezeshwa hatuwezi kuwapata wala kusonga mbele, sasa niweke akiba ya maneno, lakini nitalisimamia” aliongeza.

 Akizungumzia mashindano hayo, Meya Mwita alisema kuwa waamuzi wa mchezo huo (Marefa) wanapaswa kutenda haki bila kuwepo hali ya hujuma na kwamba anayestahili kupata tuzo hiyo ndio apatiwe.

Alisema wapo baadhi ya waamuzi wa michezo mbalimbali sio waminifu na kwamba wamekuwa na tabia ya kupanga matokeo , hivyo akaonya kwa kusisitiza kuwa jambo hilo kwenye mashinda hayo lisijitokeze.

“ Waamuzi naomba muwe waminifu, ili muweze kujenga imani kwa watu ambao mko nao hapa, jambo la kupanga matokeo sio zuri, hivyo aliyestahili kushinda ndio apewe nafasi hiyo nasio kupindisha matokeo” alisema Meya Mwita.

Hata hivyo katika hatua nyingine aliwataka wachezaji wote walioshiriki michuano hiyo, kuzingatia sheria na kuwaheshimu walimu wanaowafundisha ili kujenga nidhamu bora ya mchezo huo.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com