Godbless Lema: Yeriko Nyerere amekamatwa au ametekwa?

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema ameuliza swali je, Yeriko Nyerere amekamatwa au ametekwa?
 
Lema ameuliza swali hilo katika ukurasa  wake wa Twitter leo na kuongeza: “Msiogope. Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. "
 
Yeriko anayefahamika kuwa ni kada wa Chadema, amekamatwa leo saa tisa alfajiri na watu wanaodhaniwa kuwa ni polisi akiwa nyumbani kwake, Kigamboni, Mbutu.
 
Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amethibitisha kukamatwa kwa Yeriko.

Yerico amekamatwa au ametekwa ? MSIOGOPE. Kwani imeandikwa "Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea "


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com