Godbless Lema: Sijapenda kitendo cha Ubaguzi Nilichofanyiwa Msibani Arusha


Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Godbless Lema ametoa masikitiko yake na kuonyesha kuumizwa na kitendo alichofanyiwa leo wakati wa kuaga miili ya wanafunzi, walimu na dereva waliofariki katika ajali ya basi.


Lema anasema kitendo cha yeye kama Mbunge wa Arusha mjini pamoja na Meya wa jiji kunyimwa nafasi japo ya kutoa pole kwa familia na wafiwa wakati wa kuaga miili hiyo ni ubaguzi mkubwa."Ninamshukuru Makamu wa Rais kuja kutoa pole kwa watu wa Arusha. Leo ni ubaguzi mwingine katika Taifa Mbunge na Meya kwa kunyimwa nafasi ya kutoa pole" alisema Goodbless Lema


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com