Godbless Lema: kuwa mpinzani Tanzania inahitaji uvumilivu

Mbunge Godbless Lema amedai kuwa mpinzani wa siasa za bongo ni kazi ngumu sana, Mh Lema amesema hayo baada ya baaadhi ya watu kumdhihaki alipotoa shukrani zake kwa Mbunge Lazaro Nyalandu kufuatia kuwasaidia majeruhi wa ajali ya basi la Lucky Vicent.

Jana baada ya Mbunge Godbless Lema kumshukuru Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) Lazaro Nyalandu kuna kundi la watu liliibuka na kuanza kutoa maneno ya dhihaka kwa Lema huku wengine wakipongeza na kusema ni jambo la kheri kwa mbunge huyo kutambua kazi iliyofanywa na Nyalandu, lakini baada ya mijadala hiyo kuzidi kuwa mikuba aliibuka Mh. Lema na kutoa kauli hii kumjibu mtu mmoja ambaye alikuwa akimdhihaki.

"Kuwa mpinzani wa siasa Tanzania ni kazi ngumu sana, ila hatukati tamaa kwa sababu upendo wetu ni mkuu kuliko dhihaka. Mungu akubariki" aliandika Godbless Lema


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com