Dada wa kazi akutwa chumbani mwake ameuawa kwa kisu cha kifua

Dada wa kazi aliyetambulika kwa jina la  Christina Mabuga (37), amekutwa ameuawa ndani ya chumba chake, huko Moshi Baa, Gongo la Mboto, Dar es Salaam kwa kujichoma kisu kifuani.
Jeshi la Polisi katika mkoa wa kipolisi Ilala limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, lililofanyika katika nyumba ya mwajiri wa dada huyo wa kazi, ambapo mpaka sasa haijafamika chanzo cha dada huyo kujiua.
Mwajiri wa binti huyo, Anna Kasanda alisema alipokea taarifa saa 9:00 alasiri kwamba kuna tatizo nyumbani kwake, na ndipo alipoamua  kurudi nyumbani na kukuta mfanyakazi huyo amejiua.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com