CUF Yaomboleza Msiba wa wanafunzi Arusha kwa Bendera Nusu Mlingoti

Chama cha Wananchi (CUF) kimeungana kuomboleza pamoja na kutoa salamu za rambi rambi kwa familia za marehemu 36 wakiwemo wananfunzi 32 wa shule ya awali na msingi ya Lucky Vincent pamoja na waalimu watatu na dereva mmoja waliofariki dunia katika ajali iliyotokea wilaya ya Karatu mkoani Arusha Mei 6, 2017,.
Mkurugenzi wa Habari Taifa wa chama hicho, Salim Bimani amesema katika kipindi hiki cha maombolezo CUF itaendelea kupeperusha bendera zake nusu mlingoti hadi jumatano ya Mei 10 mwaka huu.
“CUF tunaungana na familia zote za marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awapokee marehemu kwa rehema zake. Awape subira wafiwa wote na majeruhi waweze kupona haraka,” amesema.
Aidha, Bimani ameitaka serikali kubuni njia mbadala za kudhibiti ajali ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya watanzania kila mwaka, pamoja na askari wa barabarani kusimamia sharia kwa vyombo vyote vya usafiri hasa vinavyobeba abiria ili kuepusha ajali.
Na Regina Mkonde   


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com