Chadema: Serikali iwalipe walioathiriwa na CDA


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya kati kimeitaka serikali kuwalipa fidia wakazi wa Manispaa ya Dodoma ambao kwa namna moja au nyingine wameathirika  wakati Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ilipokuwa ikifanya kazi kwa kuporwa ardhi yao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni wa Chadema, Benson Kigaila wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa.

Kigaila amesema kuwa Rais John Magufuli hawezi kuivunja CDA na ikawa ndiyo mwisho wake bila kuangalia madhara yaliyosababishwa na mamlaka hiyo kwa wananchi katika kipindi chote cha miaka 44 iliyofanya kazi.

Amesema fidia hiyo ni lazima ilipwe na serikali kuu ambayo ndiyo iliyoiweka CDA madarakani na siyo kuliachia jukumu hilo Manispaa ya Dodoma kwa kuwa haihusiki na unyang’anyi huo.

"Kuivunja CDA siyo hoja. Hoja inayokuja hapo ni je wananchi wa Dodoma walionyang'anywa ardhi yao na CDA bila kulipwa fidia watafidiwaje au ndiyo wataachwa waendelee na maumivu yao?" amesema Kigaila


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com