Bunge lachangia Milioni 100 Msiba wa Wanafunzi Arusha

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limechangia shilingi milioni 100 kwa wafiwa wa wanafunzi 32 na waalimu 4 pamoja na dereva mmoja,  waliofariki dunia katika ajali ya basi iliyotokea Jumamosi ya Mei 6, 2017 wilayani Karatu mkoa wa Arusha.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo wakiwa bungeni wamekubaliana kwa kauli moja kuwa posho za kila mbunge kwa siku ya leo zipelekwe kwa wazazi wa wanafunzi waliofariki kwa ajali ya basi la Shule ya awali na Msingi ya Lucky Vincent
Bunge kwa ujumla limechangia shilingi milioni 100, milioni 86 zimetokana na michango ya wabunge katika kikao cha leo ambapo wameamua posho zao ziende kwa wafiwa hao, huku Bunge lenyewe limetoa milioni 14.
Na Regina Mkonde


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com