Breaking News: IGP Simon Sirro Kaongea na Waandishi wa Habari kwa Mara ya Kwanza

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro kwa mara ya kwanza amefanya mazungumzo maalum na wanahabari jijini Dar es Salaam na kutangaza dau nono la Sh10 milioni kwa atakayetoa taarifa kuhusu mauaji ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga. 

“Niwaambie ukweli kuwa katika hili, maneno yatakuwa machache lakini vitendo vitakuwa vingi zaidi,” amesema katika mkutano huo.

Pia IGP Sirro amewatangazia kiama madereva wa bodaboda na kuwataka kuacha kuvunja sheria za barabarani kwa makusudi.

“Huu ni wakati wa kutii utawala wa sheria bila shuruti na nimeshaongea na makamanda wa polisi nchi nzima,” amesema 


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com