Breaking News: Halima Mdee aadhibiwa kwa Kumtukana Spika, Adhabu yake hii hapa

Kutoka Bungeni Dodoma leo May 2, 2017, Mbunge wa Kawe Halima Mdee amepewa adhabu ya kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyobaki kuanzia leo. Adhabu hii imetolewa baada Mbunge huyo kutumia lugha ya matusi dhidi ya Spika Job Ndugai na Naibu Waziri wa Afya Hamis Kigwangallah.

Kamati ya Bunge pia imemsamehe Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe baada ya kukiri kosa la kudharau Mamlaka ya Bunge April 4, 2017. Mbunge mwingine ni Ester Bullaya ambaye amepewa karipio baada ya kukiri kosa lake sawa na Mbowe.

BAADA YA MJADALA

Kupitia vikao vya Bunge la Bajeti linaloendelea Makao Makuu Dodoma, leo Jumanne Wabunge wa pande zote bila kujali itikadi za vyama vyao, wamemwomba Spika kutoa msamaha kwa Mbunge Halima Mdee aliyepewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyobakia.
Baada ya Wabunge kwa umoja wao kuomba kiti cha Spika kutompa adhabu hiyo Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA, Bunge limetangaza kumsamehe na ataendelea na vikao kwa sharti la kutorudia tena kosa.JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com