Binti wa miaka 18 atuhumiwa kunyonga na kukizika kichanga chake

Katika hali isiyo ya kawaida Binti mmoja aliyejulikana kwa jina la Latifa Vedasto anaeishi katika mtaa wa Ntungamo kata ya Buhembe manispaa ya Bukoba mkoani Kagera anadaiwa kumnyonga mtoto wake aliyejifungua siku tatu zilizopita na kisha kumzika bila kumjulisha mtu yeyote.
Kufuatia tukio hilo, jeshi la polisi linamshikilia binti huyo mwenye umri wa miaka 18 kwa uchunguzi zaidi baada ya kufukua shimo alilokuwa amezikwa kichanga huyo.
Latifa Vedasto alipohojiwa na Mtendaji wa kata hiyo amesema alimjulisha bibi yake kile kilichokuwa kinaendelea ambapo anasema alijifungua salama lakini usiku wa kuamkia May 14 mwaka huu alikuta mtoto wake amefariki dunia na ndipo alipoamua kwenda kumzika.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com