Bibi kizee apandishwa kizimbani akidaiwa kuiba gari

Fatuma Mohammed (70) na Aziz Njakula (36) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya wizi na kupatikana na gari la wizi aina ya Toyota Hiace.

Wakili wa Serikali, Hamisi Said amedai leo (Jumatatu) mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa Julai 9, 2015 eneo la Mnazi Mmoja walitenda kosa la wizi wa gari hilo mali ya kampuni ya Choice Motors.

Januari 26, 2016 eneo la Nzasa, Dar es Salaam Mohammed anadaiwa alikutwa akiwa na gari la wizi nyumbani kwake.

Baada ya kusomewa mashtaka washtakiwa wamekana na upande wa Jamhuri ulidai upelelezi haujakamilika.

Hakimu Simba ametoa masharti ya dhamana kwamba wawe na wadhamini wawili kila mmoja ambao watasaini bondi ya Sh10 milioni. Walikamilisha masharti na kuachiwa kwa dhamana.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com