AUDIO: Dakika 17 za Mbunge wa Makete Bungeni kuhusu shamba la Mifugo la Kitulo

Wizara ya kilimo mifugo na Uvuvi imetakiwa kutoa kauli bungeni ni lini itaendeleza shamba la mifugo la Kitulo lililopo wilayani Makete mkoani Njombe ili liwe na manufaa ya kutosha kwa wananchi wa makete na taifa kwa ujumla

Akichangia bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha 2017/2018 Hii jana jumamosi Bungeni Dodoma mbunge wa jimbo la Makete Prof Norman Sigalla amesema endapo waziri wa kilimo mifugo na uvuvi hatatoa majibu ya kumridhisha basi atashika shilingi

Amesema shamba la Kitulo linauwezo wa kuchukua ng'ombe 4,500 lakini mpaka sasa lina ng'ombe 750 tu licha ya waziri aliyekuwepo wakati huo Mwigulu Nchemba kufika katika shamba hilo na kuahidi kutolewa bilioni 7.6 lakini mpaka sasa hakuna utekelezaji wa hilo
  
Aidha Mbunge huyo ameiomba serikali kuangalia kwa jicho la pekee wakulima wa wilaya ya Makete hasa wa Viazi na Pareto ambao amesema hawanufaiki kwa kiwangi kikubwa na kilimo hicho kwa kuwa bado hali ya soko haiko vizuri kwao

Amesema nchi jirani ya Kenya inakuwa vizuri kwa kilimo cha viazi kwa kuwa wamejipanga vizuri ili hali wapo wakulima wa viazi katika wilaya ya Makete ambao pia wanahitaji kutoka kwa kusaidiwa na serikali

Unaweza kumsikiliza vizuri kwa kubonyeza play hapo chini:-


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com