Atupwa jela miaka 7 kwa kubaka Mtoto

Mahakama ya wilaya ya Mwera imemhukumu kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 7 mshtakiwa Abdallah Makuye Shaabani (31) mkaazi wa hawai mwera baada ya kutiwa hatiani mahakamani hapo kwa kosa la kubaka.
Imedaiwa mahakamni hapo na muendesha mashtaka Arafa Salim Mbele ya hakimu Naila Abdul basti kwamba mnamo tarehe 11/3/2015 majira ya saa 5:35 za asubuhi huko Hawai mwera wilaya ya kati Unguja bila ya halali na kwa maksudi alimbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12 jina limehifadhiwa huku akijua jambo hilo ni kosa kisheria.
Baada ya kukamilika kwa ushahidi, mahakama ilimuamuru mtuhumiwa huyo kwenda chuo cha mfunzo kwa muda wa miaka 7 ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama hiyo.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com