Apigwa na polisi hadi kufa baada ya kukutwa anakunywa kiroba

Jeshi la Polisi mkoani KILIMANJARO linadaiwa kumpa kipigo kilichomsababishia kifo bwana Furajha Mkanza wakati walipomkuta akinywa kiroba kinywaji ambacho kimepigiwa marufuku.


Taarifa zimesema Polisi hao wakiwa katika operesheni maalumu, walimkuta mwananchi huyo akinywa kinywaji hicho ndipo walipompiga hadi kumvunja mguu na kisha kuondoka naye.


Baada ya kipigo hicho Polisi hao  walimpeleka  Hospitali ya Ngoyoni ambapo aliwekewa POP ‘bandeji ngumu’ na kulazwa hadi Aprili 14 aliporuhusiwa kurudi nyumbani ili aendelee kujiuguza”, alisema mkazi mmoja.
Hata hivyo, Mei 4, akiwa nyumbani hali yake ilibadilika ghafla na baadaye kufariki dunia, Suala ambalo liliwafanya ndugu zake wachachamae na kugoma kumzika wakitaka kupeleka maiti yake kituo cha Polisi.
Chanzo:zanzi24

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com