Aliyemuua Samira kwa kumtia karoni apandishwa kizimbani

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi limempandisha kizimba cha mahakama ya Vuga mtuhumiwa Azizi Mbaraka Ali (27) mkaazi wa Meli nne Taveta kwa tuhuma za kutenda  kosa la kuua kwa makusudi.
Imedaiwa mahakamani hapo na muendesha mashtaka Suleiman Maulid mbele ya hakimu Isaya Kayange kuwa mtuhumiwa huyo amedaiwa kufanya kosa hilo tarehe 17/6 2015 huko Kiembe samaki Mkoa wa mjini magharibi Unguja ambapo alimuua Samira Sultani Abdallah jambo ambalo ni kosa kisheria.
Mtuhumiwa hakutakliwa kujibu lolote na amepelekwa rumande hadi tarehe 1/6 mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.
Itakumbukwa kuwa mifupa ya marehemu huyo ilikutwa ndani ya shimo la karo na wazamia lulu mwezi machi mwaka huu.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com