Aliyemfungia mlango mpangaji wake akiona cha moto

Mahakama ya wilaya ya Mkokotoni imempandisha katika kizimba cha mahakama hiyo mtuhumiwa Mwanahija Khamis Juma 30 mkaazi wa Mto wa pwani wilaya kaskazini A.
Imedaiwa mahakamani hapo na muendesha mashtaka wa Polisi Omar Mohd mbele ya Hakimu Muhammed Subeti kwamba siku ya tarehe 10 mwezi huu majira ya saa 1o jioni mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakani hapo kwa kosa la uvunjifu wa amani ambapo mtuhumiwa huyo alimfungia mlango mpangaji wake Jamila Juma mkaazi wa Mkokotoni kwa madai ya kuwa anadaiwa kodi ya chumba jambo ambalo ni kosa kisheria.
Kesi dhidi ya mtuhumiwa huyo imefunguliwa mahakamani hapo na baada ya kusomewa kosa lake mtuhumiwa amekataa na kuiomba mahakama impe dhamana jambo ambalo lililkubaliwa mahakamani hapo kwa masharti ya kujidhamini yeye mwenyewe kwa vile ana mtoto mchanga na kesi yake kusikilizwa tena tarehe 22 mwezi huu  kwa upande wa mashahidi.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com