Yule Binti aliyejirusha Baharini Huyu Hapa

Abiria mrembo ambaye jina lake halikufahamika mara moja jana alijitupa kwenye Bahari ya Hindi kutoka kwenye boti iliyokuwa ikienda Unguja kutoka jijini Dar es Salaam na  baadhi ya watu wake wa karibu wamesema sababu ya kufanya hivyo.
Habari kutoka kwa watu wake wa karibu waishio mjini Kikwajuni, Unguja, Zanzibar na waliokuwa kwenye boti hiyo zinasema kuwa, mrembo huyo alijitupa baharini baada ya kufuatwa Dar es Salaam na mjomba wake  ili arudishwe nyumbani kwao kufuatia kuondoka bila ridhaa ya wazazi wake.
“Huyu binti alifuatwa na mjomba wake Dar baada ya kuondoka nyumbanai kwao Kikwajuni na kwenda kuishi kwa mtu ambaye wazazi wake hawamfahamu sawasawa.
“Sasa kinachoonekana ni kwamba, kitendo cha kurudishwa nyumbani kilimtia hasira na kuamua kujitupa baharini akiwa anarudishwa. Kwa vyovyote vile alikuwa hataki kurudi kwao, alitaka endelee kuishi kwa huyo mtu Dar jambo ambalo hakuna ndugu yake aliyekuwa akilikubali,” kilisema chanzo na kuongeza kuwa, tukio hilo liliwatia hofu abiria wengine na kuona kama ni safari  yenye mkosi.
Naye abiria mmoja aliyekuwa ndani ya boti hiyo waliyokuwa wakisafi ria ya Azam Marine Kilimanjaro alisema msichana huyo tangu alipoingia ndani ya boti, hakuwa akisema chochote, alikuwa kimya muda wote wa safari hadi alipoamua kujitupa baharini hali iliyozua tafrani kwa abiria wenzake na kuamini kuwa, alidhamiria kufanya hivyo kwa sababu alionekana mwenye akili timamu.
Hata hivyo, habari zinasema mrembo huyo baada ya kuokolewa anaendelea vizuri na ni mzima wa afya huku ndugu zake wakishughulikia kumchukua jana jioni. Wakati huohuo, taarifa  kutoka Kampuni ya Azam Marine na Kilimanjaro Fast Ferries iliyotolewa jana ilisema kuwa, abiria huyo alijitosa majini kutoka kwenye chombo hicho  cha Kilimanjaro maeneo ya Chumbe na taarifa zilipofi ka kwa nahodha ni kwamba,  chombo kilipunguza spidi  na kurudi kwa ajili ya uokozi.
“Tulifanikiwa kumuokoa abiria huyo akiwa mzima na tumemkabidhisha kwa vyombo husika tulipofi ka bandarini Zanzibar,” ilisema taarifa hiyo. Baadhi ya wanasheria walisema jana kuwa, kwa kawaida abiria huyo anatakiwa kufi kishwa kwenye mkono wa sheria kwa vile kitendo alichokifanya hakina tofauti na mtu aliyetaka kujiua kwa makusudi.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com