Yaliyojiri Mahakamani kwenye kesi ya Mume wa Shamsa Ford

Leo April 4, 2017 ambapo mume wa mwigizaji wa filamu Shamsa Ford aiitwae Chid Mapenzi alifikishwa Mahakama ya Kinondoni kufuatia kuitwa Polisi kwa sakata la dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa wakili wake aitwae Reuben Simwanza  ameiambia millardayo.com kuwa kesi imeahirishwa mpaka tarehe 13  mwezi April kwa kosa la matumizi ya dawa hizo.

‘Kwa kifupi ni kweli kesi imekuja leo Mahakama ya Kinondoni amesomewa shtaka kwa mara ya kwanza kuhusu sheria ya madawa ya kulevya na usafirishaji wa madawa haramu, kimsingi madawa  yalitajwa kwa lugha inayoeleka ni marujuana huku mshtaki amekana mashtakiwa hayo hiyo yuko nje kwa dhamana na kesi itatajwa tena tarehe 13/4/2017 ndio atarudi Mahakamani’- Wakili


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com