Watu Tisa Wanahofiwa Kufa Maji Zanzibar

WATU tisa hawajulikani waliko huku 44 wameokolewa baada ya mashua yao ya uvuvi kuzama pwani mwa kisiwa cha Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Upelelezi  amesema harakati za uokoaji bado zinaendelea.
“Tunafahamu, kuwa ajali hiyo ilisababishwa na upepo na mawimbi makali yaliyosababisha mashua hiyo kuzama,” alisema.
Manusura mmoja aliwaambia waokoaji kuwa takriban watu 53 waliondoka kwenda kuvua samaki jana jioni wakati bahari ilikuwa tulivu lakini hali ya hewa ilibadilika na kusababisha mawimbi makali na kwamba hajawaona wenzake tangu ajali hiyo itokee.
Uvuvi ni shughuli kubwa ya kiuchumi kisiwani Zanzibar lakini mashua nyingi zimechakaa na hivyo husababisha ajali nyingi kila mara.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com