Washtakiwa 61 watishia Kugoma

Arusha. Washtakiwa 61 wanaokabiliwa na kesi 15 tofauti za ugaidi wametishia kutohudhuria mahakamani hadi upelelezi utakapakamilika.

Tishio hilo limekuja baada ya kuandika barua kwenda Ofisi ya Hakimu Mfawidhi mkoani Arusha iliyoandikwa na Yasin Sanga kwa niaba yao.

Barua hiyo  inaeleza kuwa tangu mwaka 2014 walipokamatwa kesi hazijaanza kusikilizwa.

Barua hiyo ilipitia kwa Mkuu wa Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha.

Mshtakiwa Sanga katika barua hiyo yenye kumbukumbu namba 78/AR/I/VIII/184 ya Machi 30, ametaja sababu saba zilizosababisha wagome ikiwamo kuchoshwa na mambo yanayoendelea kwenye kesi hiyo.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com