Wanaowapekua wafanyakazi Sehemu za Siri Kukiona

Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde amesema Serikali itawachukulia hatua waajiri wa migodini wanaowadhalilisha wafanyakazi kwa kuwapekua hadi sehemu za siri, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Mavunde alikuwa akijibu swali bungeni mjini Dodoma leo kuhusu msimamo wa Serikali dhidi ya matukio ya udhalilishaji wa wafanyakazi maeneo ya migodini.

Naibu Waziri Mavunde amesema kumekuwa na matukio ya udhalilishaji kwa wafanyakazi yanayofanywa na waajiri zikiwamo baadhi ya kampuni za Wachina.

Amesema baadhi ya Wachina hao wamekuwa na tabia ya kusingizia kutojua Kiswahili kama sababu ya kutofahamu sheria za kazi nchini na kunyanyasa wafanyakazi wao.

Pia, amebainisha kuwa Serikali inatambua kutojua sheria si sababu ya kufanya kosa, hivyo imekuwa ikipokea taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kuhusu matukio ya udhalilishaji.

Ameahidi kuwafikisha katika vyombo vya sheria waajiri wanaoendelea kukiuka sheria za kazi nchini.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com