Viongozi wa serikali watishiwa Kuuawa


Wananchi kata ya Yaeda chini wilayani Mbulu mkoani Manyara wameiomba serikali kutoa ulinzi wa kutosha kwao pamoja na viongozi wa kata hiyo kutokana na vitisho vya kuuwawa na kundi la vijana ambao wanapinga zoezi la mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa kuwekwa mipaka kwa lengo la kubainisha maeneo ya wafugaji na wakulima katika bonde la yaeda chini huku viongozi wa serikali ya kijiji na kata hiyo wakitengwa kuunga mkono hatua hiyo ya mpango bora wa ardhi.

Eneo hili ambalo limetawaliwa zaidi na sheria za kimila linaelezwa pia kuwa na mila kandamizi kwa wanawake jambo linalowafanya kukosa uhuru wa kufanya shughuli za kimaendeleo kama jamii nyingine.

Na hawa ndiyo viongozi ambao wametengwa kwa maagizo ya viongozi wa kimila za kihardzabe kutokana na kupinga pamoja na kutoa ushahidi kwa jeshi la polisi juu ya vijana waliotekeleza zoezi la uondoaji wa alama hizo za mipaka katika kata hii ya yaeda chini .


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com