Uteuzi alioufanya Waziri Ummi Mwalimu Hii Leo

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amemteua Dk Respicious Lwezimula Boniface kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI).

Awali nafasi hiyo ilikuwa ikikaimiwa na Dk Othman Kiloloma.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa wizara, Nsachris Mwamaja ilisema, kabla ya uteuzi huo Dk Respicious Lwezimula alikuwa daktari bingwa katika Taasisi hiyo na kwamba uteuzi huo unaanza leo Aprili 5.

Ummy alisema nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa MOI ilikuwa wazi tangu mwaka 2014 baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji kustaafu kwa mujibu wa sheria.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com