Tumuenzi Kanumba kwa Vitendo


MSANII wa maigizo na vichekesho nchini, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema kuwa, wasanii wa tasnia ya filamu wanapaswa kumuenzi kwa vitendo aliyekuwa staa wa filamu Bongo, Steven Charles Kanumba ambaye leo ametimiza miaka mitano tangu kifo chake.
Steve alisema hayo leo wakati alipoungana na baadhi ya wasanii wa Bongo Movies kufanya ibada fupi ya kumuombea Kanumba kwa Mungu kutokana na matendo yake aliyowaachia kama kumbukumbu kwao. Ibada hiyo imefanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
“Leo siyo siku nzuri kwetu kama wasanii, ni siku ya majonzi, tunaamini Kanumba yupo sehemu salama huko aliko, niombe wasanii wenzangu tuwe na ushirikiano katika kumuenzi, tusimuenzi kwa visirani, sisi kama ndugu tuliokutana hapa tushikamane na familia katika kumuenzi Kanumba,” alisema Steve.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com