TFF imeirudishia Kagera Sugar point 3 vs Simba, hakuna rufaa Tena

Katibu mkuu wa shirikisho la soka Tanzania TFF Selestine Mwesigwa ametangaza maamuzi yaliyofikia na kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kuhusu Simba kupewa point 3 dhidi ya Kagera Sugar kwa madai ya kuchezeshwa mchezaji Mohamed Fakhi aliyedaiwa kuwa kadi 3 za njano.
Selestine Mwesigwa ametangaza maamuzi hayo katika makao makuu ya TFF na kusema Simba imepokonywa point tatu na hakuna nafasi ya kukata rufaa kutokana na kikao cha bodi ya Ligi kilichotoa maamuzi ya awali kilikuwa kinyume kisheria.
Msikilize kwa kubonyeza Play hapo chini:-

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com