Tazama bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika kuanzia kesho


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa zitakazoanza kutumika kuanzia kesho.

Akitangaza bei hizo leo (Jumanne)Meneja wa Mawasiliano wa Ewura,  Titus Kaguo aliwaambia wanahabari kuwa petroli imeshuka Sh 3 itauzwa Sh 2057 kutoka 2060, dizeli imepanda kwa Sh 12, kutoka Sh 1913 hadi 1925 na mafuta ya taa ni Sh 1958 kutoka 1952.

"Mabadiliko haya bei yametokana na  bei za mafuta katika soko la dunia kubadilika sanjari na mfuko wa bei na gharama za usafirishaji ikilinganishwa na mwezi uliopita,"amesema Kaguo.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com