Taarifa ya CUF kuhusu Uvamizi Uliotokea Leo

Leo Tarehe 22/4/2017 Mhe. Mkumbi aliandaa mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Vinna Hotel iliyopo Mabibo, Dar es Salaam. Mhe Mkumbi ameitisha mkutano huo akiwa ni Kiongozi Mkuu wa shughuli za Chama wilaya ya Kinondoni ili kuzungumzia masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika Wilaya yake baada ya kuwa nje ya nchi nchini Marekani kwa wiki kadhaa. 

Wakati anaendelea na Mkutano wake ghorofa ya nne (4th Floor) na waandishi wa habari takribani 25 kutoka vyombo mbalimbali vya habari ghafla kundi la wafuasi wa Lipumba walifika Hotelini hapo wakiwa na gari mbili za Chama cha CUF Land Cruiser zilizokuwepo Ofisi Kuu-Buguruni huku wakiwa wameficha sura zao kwa Soksi, wameshika silaha mbalimbali ikiwemo mapanga na mmoja akiwa na bastola na kuanza kuwashambulia waandishi wa habari na Viongozi wa CUF waliokuwepo katika mkutano huo.

 Katika kujitetea wa walinzi wa Chama pamoja na wananchi waliojitokeza kuwashambulia wavamizi hao ndipo walilazimika kukimbia kwa kupanda magari waliokuja nayo na wananchi walifanikiwa kumkamata mmoja wa mfuasi wa Lipumba waliofanya uvamizi na kumjeruhi vibaya miguuni na sehemu ya kichwani. 

Viongozi wa CUF walizuia wananchi wenye hasira wasimchome moto muhalifu huyo, hata hivyo Wananchi waliendelea kuwashambulia wahalifu na kuvunja vioo vyote vya magari hayo na kukimbia. Waandishi wote waliojeruhiwa wametoa maelezo yao kituo cha Polisi Magomeni.

MSIMAMO NA TAMKO LA CHAMA CUF JUU YA TUKIO HILO:
1. CUF Tunalaani vikali kitendo hicho kilichofanyika na kundi la Lipumba kwa uratibu wa Abdul Kambaya, BG Fadhili na Masoud Mhina kwa Baraka zote Profesa Ibrahim Lipumba. 

Kitendo hicho si cha kiungwana na hakiashirii nia njema, uvumilivu na uendeshaji wa siasa za kistaarabu. Kama Katibu wa Wilaya Mzee Mkandu juzi tarehe 19/4/2017 alifanya Mkutano kama huo kwa amani bila bughudha na watanzania walisikia alichokizungumza, iweje Mwenyekiti wake wa Wilaya ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa afanyiwe vurugu hizo? 

2. Iweje Jeshi la polisi Limuachie Lipumba kuratibu kundi la wahalifu bila ya kuchukuliwa Hatua za kisheria? Hivi hata kama mathalani mkutano ule haukuwa halali, hii ndio njia sahihi ya kuzuia kutofanyika kwake? Iweje Jeshi la Polisi linabariki kitendo cha uharibifu wa mali za raia mwema mfanyabiashara wa Hotel ambaye analipa kodi kwa serikali huku ikiacha kuwachukulia hatua zinazostahiki wahalifu hao?

3. Tunatoa pole kwa waandishi wote wa habari waliojeruhiwa katika tukio hili linalopaswa kulaaniwa na kila mpenda haki na demokrasia nchini na CUF itaendelea kuwa pamoja nanyi kuhakikisha kuwa mnarejea katika hali yenu njema ya afya ili kutekeleza majukumu yenu ya kuwatumikia Watanzania.

4. Tunalitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kuwakamata wahusika wote wa tukio hilo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria (mahakamani). Matukio kama haya yanayofanya na kundi la llipumba yamekuwa yakijirudia mara kwa mara ikiwemo jaribio la Utekaji kwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Mhe. Joran Bashange mbali na wahusiaka wanne (4) kukamatwa eneo la tukio lakini Tunasikitika kuona Jeshi la polisi Mkoa-ZCO, na DPP wamekalia mashtaka hayo na kushindwa kuchukua hatua za kisheria. Tunalitahadharisha Jeshi la Polisi kutekeleza wajibu wao wasusibiri machafuko na maafa makubwa zaidi yatokee. Na orodha ya matukio hayo tumeiambatanisha na taarifa hii.

5. Tunamtahadharisha Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Franscis Mutungi na Profesa Lipumba kuwa wao watawajibika juu ya athari na machafuko makubwa zaidi ikiwemo mauaji yatakayojitokeza kwa kushindwa kuheshimu sheria na kuchochea ufanyikaji wa vurugu hizi. Lipumba amekne ya kufanya.

6. Mheshimiwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), hakuna maslahi yeyote unayoweza kuyapata kwa kuendelea kubariki ufanyikaji wa vitendo hivi vya uvunjifu wa amani katika nchi yetu zaidi ya kuendeleza kujengwa Chuki zaidi kati ya Jeshi la Polisi na raia wema, wananchi pale linaposhindwa kuwatendea haki wananchi wote kwa usawa. IGP chukua hatua utasababisha mauaji. Kwa kuwalinda wahalifu.

7.  Tunatoa wito kwa Jukwaa la Wahariri wa Habari nchini kuchukua hatua dhidi ya Lipumba na kundi lake ambao sasa wamehamia kuwadhuru waandishi wa habari na kutoa lugha za vitisho pale zinaporipotiwa taarifa kinyume na matakwa yao. Baada ya kuendesha vitendo hivi kwa muda mrefu sasa kwa viongozi na wanachama wa CUF wakati mwingine ndani ya Mahakama Kuu.

HAKI SAWA KWA WOTE
MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI
NA MAHUSIANO NA UMMA
MAWASILIANO:
0784 001 408 Airtel | 0767 062 577 Vodacom
Imetolewa Leo Tarehe 22/4/2017


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com