Sirro: Wenye tuhuma dawa za kulevya wafike kituoni wenyewe

Kamishina wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amewataka wote walioitwa polisi ili kuhojiwa kwa tuhuma za dawa za kulevya, wafike kituoni hapo mara moja.

Kamishina Sirro amesema hayo leo (jumatano) wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema ni vyema watu hao wakaripoti ili kama hawana hatia wasafishwe au wakikutwa na hatia wapelekwe mahakamani kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria.

"Niwaombe waliopokea wito wa polisi waje wahojiwe kwa sababu mtu akija mwenyewe inasaidia tofauti na anaposubiri nguvu ya dora kutumika kumkamata ambapo lolote linaweza kutokea hasa kwa yule anayekataa hata kukamatwa." amesema Siro


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com