Shilole Ajivisha Pete ya Uchumba

STAA wa Filamu za Kibongo, Zuwena Mohammed ameamua kujivisha pete ya uchumba mwenyewe, kitendo ambacho kimezua minong’ono kwa watu wengi wakidai kuwa amevishwa na mtu ambaye hajamuweka wazi.

Akizungumza na Ijumaa, Shilole alisema kuwa aliwahi kuvishwa pete na aliyekuwa mpenzi wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, ikapotea kitatanishi kisha Nuh akaoa mwanamke mwingine hivyo akaona kuliko kidole hicho kibaki tupu, akisitiri.

“Pete ile ya Nuh ilipotea, sijui huwa ni za mashetani? Nimeona ninunue nyingine niivae, hakuna cha mwanaume wala nini, mimi sijaona tatizo kuivaa na huenda ndiyo naiita ndoa,” alisema Shilole.

Chanzo: Gazeti la Ijumaa


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com