Polisi aeleza alivyomuhifadhi mshtakiwa

Askari wa Jeshi la Polisi, Sajenti Dismas Ngalaba (50) ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jinsi alivyomuhifadhi mshtakiwa Manase Philemon mahabusu katika kituo cha Kijitonyama.

Aliongozwa  na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi kutoa ushahidi katika kesi ndogo ndani ya shauri la msingi linalomkabili raia wa China maarufu malkia wa meno ya tembo Yang Feng Glan (66) na wenzake wawili.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi shahidi huyo alidai Aprili 20, 2014 kati ya saa tisa na saa 12:00 jioni alikuwa ofisini Kituo cha Polisi Kijitonyama.

Alidai saa 9:45 jioni afande Beatus alifika kituoni hapo akiwa na Manase na kuingia naye kwenye ofisi ya mkuu wa upelelezi ambako walikaa kwa dakika tano.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com