Picha zote za Vurugu kuibuka katika mkutano wa wanahabari Mabibo jijini Dar es salaam


 Vurugu imetokea leo  wakati kundi la watu wanaodaiwa kuwa wanachama wa chama kimoja cha siasa (jina kapuni hadi itapothibitishwa) kupambana na  wenzao wanaosadikiwa kuwa wapinzani wao baada ya kundi moja kuvamia mkutano wa upande mmoja  na waandishi wa habari katika Hotel ya Vinna Hotel maeneo ya  Mabibo jijini Dar es salaam, na kuzua taharuki kubwa kwa waandishi wa habari na wakaazi wa eneo hilo.  

Mashuhuda wamesema watu kadhaa wasiojulikana walifika hapo wakiwa wamefunika nyuso zao kwa vitambaa huku wakiwa na silaha za jadi na kuanza vurugu.

Baada ya mkutano kuvurugika baadhi ya  waliokuja kufanya vurugu walikimbia huku wakikimbizwa na wanachi wenye hasira kali ambao walifanikiwa kumkamata mmoja wao na kumjeruhi  kwa kumkata maungio ya kisigino ya mguu wake wa kulia.

Juhudi za kuwapata wasemaji wa pande mbili hizo zinaendelea
Mmoja wa watuhumiwa wa uvamizi akiwa chini ya ulinzi mara baada ya kudhibitiwa na na wananchi kisha kumkata mguu na kushindwa kutembea 
Mtuhumiwa akiwa amekatwa mguu wa kulia akiugulia maumivu  baada ya kujeruhiwa

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com