Nape amjibu Prof. Shivji kwa Kitendo cha Kuwakanyaga wanawake

Ikiwa ni siku moja tu baada  ya Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Mtwara kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Nape Nnauye  kulakiwa kimila na baadhi ya wafuasi wake wakiwemo akinamama walioonekana kulala chini na kisha Mbunge huyo ambaye kwa sasa ameendelea kujihimalisha zaidi kwenye medani za kisiasa za ‘kipekee’ baada ya kuondolewa Uwaziri wa Serikali ya awamu ya tano, ameibuka na kumjibu Profesa Issa Shivji kufuatia tukio hilo  ambalo Prof. Shivji alitoa ushahuri.
Kupitia ukurasa wa twitter wa  Prof. Shivji majira ya jioni alibandika picha ya Nape akionekana kupita juu ya Wanawake hao waliokuwa wakimlaki kimila na kuandika:  Angekataa. ‘Nawashukuru sana mama zangu. Nilijitolea kuwahudumia, kuwa chini yenu kama mtoto wenu, sio kuwakanyaga’.
 Hata hivyo baada ya andiko hilo la Profesa Shivji, watu mbalimbali walipata kutoa maoni yao kuhusiana na tukio hilo ikiwemo mila na tamaduni za Mtanzania ambazo zipo toka enzi. (tazama picha chini). Lakini  baada ya kupita saa moja tokea kuweka andiko hilo, Nape kupitia kurasa wake wa twitter aliweza kumjibu Profesa Shivji, ambapo aliandika: Kwa mila za kusini tendo hili ni la heshima KIMILA na ukikataa ni sawa na DHARAU KUBWA kwa waliokufanyia, hata hivyo ndio maana NILILIZWA!.
Hata hivyo MO Blog imeshuhudia mjadala huo ukipamba moto hasa kupitia mitandao ya kijamii kwa kila mmoja akijadili jambo hilo kwa namna anavyojua yeye juu ya mila hizo.
Ukurasa wa twitter wa  Prof. Shivji aliobandika ujumbe huo

Picha aliyotupia Nape kupitia kurasa wake wa twitter aliweza kumjibu Profesa Shivji, ambapo aliandika: Kwa mila za kusini tendo hili ni la heshima KIMILA na ukikataa ni sawa na DHARAU KUBWA kwa waliokufanyia, hata hivyo ndio maana NILILIZWA!.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com