Mwili wa Tshisekedi kurejeshwa nyumbani Mei 12Jeneza lililobeba mwili wa Etienne Tshisekedi.Haponi Brussels nchini Ubelgiji
Mwili wa kiongozi Mkuu wa chama cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Ettiene Tshisekedi, utarejeshwa nyumbani tarehe 12 mwezi ujao.
Tarehe hiyo imetangazwa na chama chake cha UDPS baada ya mashauriano na familia yake.
Tshisekedi alifariki dunia mwezi Februari akipewa matibabu jijini Brussels nchini Ubelgiji.
Akitoa tangazo hilo jijini Kinshasa siku ya Jumamosi, Katibu Mkuu wa chama hicho Jean-Marc Kabund ameongeza kuwa Tshisekedi huyo atazikwa katika Makao Makuu ya chama cha UDPS katika jiji hilo.
Kumekuwa na mvutano kati ya serikali na chama hicho ni wapi mwanasiasa huyo azikwe lakini, upinzani umesema hautaki pendekezo la serikali kuwa Tshisekedi azikwe katika makaburi ya umma Gombe.
Aidha, Kabund ametaka serikali ya Kinshasa na MONUSCO kushirikiana kuhakikisha kuwa kuna usalama wa kutosha wakati mwili wa kiongozi wao utakaporejeshwa.
Kiongozi huyo hajazikwa kwa sababu muungano wa upinzani aliokuwa anaongoza, ulitaka kuanza kutekelezwa kwa mkataba wa kisiasa uliotiwa saini mwaka uliopita kabla ya mwanasiasa huyo azikwe.
Upinzani umesema hautambui uteuzi wa Bruno Tshibala kuwa Waziri Mkuu, baada ya kuteuliwa na Rais Joseph Kabila.
Chanzo: RFI


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com