Mwalimu ahukumiwa kwa mshahara hewa


MAHAKAMA ya Wilaya ya Geita, mkoani Geita imemhukumu Mwalimu Onyango Nguka kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya Sh. 500,000 na kurejesha Sh. milioni 3.9 alizoisababishia hasara halmashauri ya mji wa Geita.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya wilaya, Ushindi Swallow, baada ya kujiridhisha na ushahidi wa pande zote mbili.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Kelvin Msururi, akisaidiana na Augustino Mtaki na Felsta Chamba, walidai mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi 13, 2014 hadi Novemba 30, 2014.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alikuwa mwalimu katika Shule ya Sekondari Geita, alitoweka kituoni kwake Machi 13 na Novemba 2014, lakini aliendelea kupokea mshahara bila kuwapo wala kufanya kazi kwa kulipwa Sh. 3,974,542.50.

Mshtakiwa akitetewa na wakili, Neema Chritian, alipotakiwa kujitetea aliiomba mahakama kumuonea huruma kwa sababu alikuwa na wazazi na watoto wanao mtegemea.

Akitoa hukumu hiyo, hakimu Swallo aliamru mshtakiwa kufungwa gerezani miezi 12 au kulipa faini ya Sh. 500,000 na kuzirejesha  Sh. 3,974,542.50 alizosababisha  hasara serikali. Mshtakiwa alinusurika  kwenda gerezani baada ya kulipa  faini hiyo.

Hukumu hiyo ni ya pili kutolewa na mahakama hiyo ya watumishi hewa kulipwa mshahara, Agosti 24, mwaka jana mtuhumiwa mwingine  Henrry Tagata aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Msalala, wilayani Nyang’hwale, alihukumiwa kwenda gerezani miaka miwili au kulipa faini ya Sh. 800,000 na kurejesha Sh. 9,698,618.80 aliyoisababishia hasara serikali.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com