Mvua zaharibu barabara Iringa, Wakazi wake walalamika

Image result for barbara maketeWakazi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa mkoani Iringa wamelalamikia kero ya baadhi ya barabara kutopitika kutokana na kuharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.
Hali hiyo ambayo imekuwa kikwazo kikubwa kwa wananchi wa kawaida na wasafirishaji wa mabasi madogo ya abiria imekuwa ikijirudia mara kadhaa ktk manispaa ya Iringa hasa ktk kipindi cha mvua.
Kufuatia kilio hicho cha muda mrefu cha ubovu wa barabara Manispaa hiyo imeingia mkataba na makampuni ya ukandarasi kwa ajili ya matengenezo ya barabara 15, ikiwemo hii ya Mtwivila kwa lengo la kuziwezesha barabara nyingi kupitika wakati wote huku makandarasi wakiomba kulipwa pesa za kazi wanazoomba kwa wakati.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com