Mvua yauwa wanafunzi wawili na kujeruhi wanne

Wanafunzi wa wawili wa shule ya Msingi Kasoli, ambao ni ndugu wa familia moja wamefariki dunia, huku watu wengine wanne wakijeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa Kanisa la AIC Kasoli wakati wakiwa wamejikinga na mvua Kanisani hapo iliyokuwa ikinyesha na kuambatana na upepo mkali.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, BONIVENTURE MUSHONGI amesema ajali hiyo ilitokea Aprili 24 saa 12 jioni katika Jiji na Kata ya Kasoli Tarafa ya Mhango Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, ambapo baadhi ya majeruhi wamelazwa katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu na hali zao zinaendelea vizuri.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com