Mpanda baskeli agongwa na gari na kufariki

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina Salum Khamis Salum (73) mkaazi wa Betrasi Zanzibar amefariki Dunia baada ya kugongwa na gari alipokua akiendesha baskeli na kisha gari hiyo kukimbia bila kufahamika namba za usajili wala dereva aliyekua akiendesha gari hiyo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi kamishna msaidizi muandamizi wa polisi Hassan Nassirr Ali amesema kuwa kitendo alichofanya dereva huyo kukimbia baada ya ajali hiyo kutokea si cha kiungwana kusema kuwa watafanya upelelezi kuhakikisha wanamtia mikononi.
Mwili wa marehemu huyo ulipelekwa hospitali ya mnazi mmoja kwa uchunguzi uliofanywa na mganga mkuu wa hospitali hiyo na kuonesha kuwa  ameumia kwa ndani ya moyo jambo ambalo lilipeleka kupoteza maisha.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com