Mapovu ya Mbowe baada ya Chama Chake Kukosa Wabunge Bunge la Afrika Mashariki

Chama cha CHADEMA tutakwenda kuitafuta haki pengine, Kama Taifa tungetegemea kupata wawakilishi wa Taifa na tuwe tumemaliza Uchaguzi huu wa kuwapata wawakilishi wetu kwenye Bunge la Afrika Mashariki.

Lakini ndio kwanza kwa matokeo haya na kwa utaratibu huu wa upindishaji wa Sheria za Uchaguzi, tutakwenda Mahakamani, tutaitafuta haki hii mahali pengine.

Ni aibu kwa Taifa kwamba Chama kimoja kinataka kutafuta na kupitisha mgombea wa Chama kingine cha Upinzani, haiwezekani na haikubaliki, Spika amevunja kanuni za Bunge, Sheria hazikuheshimiwa, ubabe umetumika lakini kwetu sisi ni sehemu ya mchakato wa demokrasia tutaendelea kuitafuta haki yetu.


Nafasi mbili za Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki wapende wasipende ni za CHADEMA, tutakaa tutashauriana, hawawezi kueleza sababu za msingi za kuwakataa wagombea wetu.

Kwa sababu wagombea wetu wanasifa, lakini tunajua huu ni mkakati wa ccm , Rais anahusika, Waziri Mkuu anahusika na viongozi wao wanahusika. Wanatumia Sheria gani kutuchagulia wapinzani wawakilishi wetu katika Bunge la Afrika Mashariki?

Kama Chama nafasi zetu mbili (2), wapende wasipende zipo, Kama mtu unathamini utaifa kwanini wanawakataa? Tumeleta viongozi wazuri viongozi wenye sifa, very competent, ambao wanaweza kutuwakilisha vizuri EALA wanawapigia kura za hapana, kwa sababu ni mkakati wa ccm, sisi tunaona ni ujinga tu, wanajipaje uhalali wa kutuchagulia ni nani wawe wawakilishi wetu? Hakuna demokrasia kama hiyo duniani kote, ila kwa ujinga wa CCM kama mlivyoona na kusikia ndo maana Uchaguzi umekuwa wa kijinga, Kama Chama tunasisitiza nafasi zetu mbili zipo.

Na hakuna sababu za msingi zilizotolewa za kuwakataa wagombea wetu, who knows tomorrow? Tunaweza tukarejesha majina hayo hayo tena...The Battle has just begun!!


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com