Mama huyu Mjane yamfika Makubwa..Asimulia Kila Kitu


Mjane Farida Saleh Amrani amejitokeza mbele ya vyombo vya habari na kulalamika kudhulumiwa nyumba yake aliyoachiwa na marehemu mme wake aliyefariki mwaka 2011.

Akizungumza na kuonyesha hati halali za nyumba hiyo yenye kitalu namba 2111 iliyopo Mbezi Beach Kata ya Maliasili, Farida alisema kuwa katika nyumba hiyo walihamia mwaka 2002 na hati ya nyumba hiyo ilikuwa kwa mwanasheria kipindi chote hata pale marehemu mumewe alipofariki.

Amesema kuwa, baada ya mume wake kufariki mtoto wa marehemu mkubwa aliambiwa afungue mirathi lakini akawa anasema taratibu za kabila la kihaya ni baada ya mwaka mmoja kumalizika.

Farida ameeleza kuwa, mumewe Alfred Kyoma alifariki akiwa safarini Bukoba na amemuacha na watoto wawili ambao baada ya kumalizika kwa msiba familia nzima walikubaliana nyumba ipangishwe ili fedha zitakazopatikana ziwasomeshee watoto ambao mmoja yupo kidato cha tano sasa hivi na mwingine cha kwanza.

Nyumba hiyo kwa Yusuph Shaban Omari ambaye ni mmiliki wa Royal Village Hotel iliyopo Temeke na ameuziwa na kaka wa marehemu lakini katika hati ya mauzo ikiandikwa Alfred Athanas Kyoma akishirikiana na mtoto wa Marehemu.

Majirani wa nyumba hiyo Wamesema kuwa siku chache zilizopita waliona watu wakivunja nyumba na kuingia ndani na kutoa vitu ndani vya mpangaji anayekaa hapo ambaye alikuwa amesafiri.

Kwa sasa nyumba hiyo imewekwa mlinzi ambaye jitihada za kumwambia afungue zilishindana baada ya kugoma kuruhusu watu kuingia ndani na imeuzwa kwa kiasi cha shiliingi milion sitini (60


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com