Mama anusurika kukatwa Ulimi akiwa anaelekea Kanisani

Mwanamke mmoja ajulikanae kwa jina la Domitila Muhoza (53) mkazi wa Masanga Manispaa ya Kigoma Ujiji ameshambuliwa na mtu asiyejulikana baada ya kuvamiwa akiwa na nia ya kumkata ulimi majira ya alfajiri wakati akielekea kanisani.
Kwa mujibu wa tovuti ya MO Blog, Muhoza amesema wakati akielekea kanisani alisikia mtu akimshika kwa nyuma na kuanza kumpiga maeneo ya usoni na kutaka kumkata ulimi huku akimuomba pesa na vitu vingine vya thamani alivyokuwa navyo.
“Wakati akiendelea kunipiga aliingiza mkono mdomoni ili anikati ulimi, kilichonisaidia nilimng’ata meno ndio akanichia, licha ya kuwa alikuwa ameshaniumiza sana usoni na mdomoni na kuniambia nimpe pesa lakini sikuwa nazo nikamuachia nguo nilizokuwa nazo,” alisema Muhoza.
Aidha Muhoza alisema kuwa, hakumtutambua mtu yule kwasababu alikuwa ameshaumia ambapo baada ya mtu yule kukimbia walikuja watu na kumsaidia kumpeleka hospitali ya Rufaa ya mkoa Maweni kwaajili ya matibabu.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Maweni Daktari Fadhili Kibaya, amesema walimpokea mama huyo akiwa na hali mbaya akivuja damu mdomoni huku akiwa na majeraha sehemu za usoni ambapo alipatiwa matibabu.
“Ulimu na sehemu zingine zenye majeraha zilishonwa na kupewa dawa na mpaka sasa amelazwa akiuguza majeraha yake, hakuna athari kubwa aliyoipata kwenye ulimi hivyo tunategemea baada ya muda ulimi utapona na kuanza kufanya kazi kama kawaida,” alisema Daktari Kibaya.
Emmanuel Senny, Kigoma


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com