Makonda Aanza Kuguswa na Kitendo cha Wanahabari Kumsusia

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ameonesha kusononeshwa na kitendo cha waandishi wa Habari wengi kususia habari zake bila kujali zina manufaa gani kwa jamii

Mkuu huyo wa mkoa leo hii asubuhi wakati wa tukio la Rais John Magufuli kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Reli ya Kisasa (standard Gage) Pugu jijini Dar Es Salaam, Makonda amewataka waandishi wa habari kufanya kazi ambazo watanzania wanazitaka

"Niwaombeni ndugu zangu wanahabari fanyeni kazi zenu, leo kuna tukio kubwa kama hili la maendeleo ya taifa letu, lakini utashangaa habari zitakazopewa kipaumbele kwenye vyombo vya habari, fanyeni kazi kwa manufaa ya watanzania" amesema Makonda

Ikumbukwe kuwa wiki chache zilizopita Jukwaa la wahariri Tanzania kupitia kwa katibu wake Nevile Meena walitangaza kwa umma kususia kuziandika habari za mkuu wa Mkoa huo na kuomba waandishi wote wa habari nchini waunge mkono uamuzi huo

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com