Mahakama yamfuata mtuhumiwa wa mauji Hospitali, yamsomea mashtaka hapo hao


Licha ya mshtakiwa Goodluck Shuma kulazwa Hospitali ya Rufaa KCMC, Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi imemfuata na kumsomea mashtaka ya kuua kwa kukusudia

Shuma anatuhumiwa kwa mauaji ya askari Sajini Abdallah Fakhi aliyeuawa kwa kukatwa kwa panga Machi 17 saa 1:30 usiku na kundi la watu wanaodaiwa kumpigia kelele za mwizi, alipoingia kwenye nyumba eneo la Msaranga.

Juzi, upande wa mashtaka uliwasomea makosa washtakiwa sita, lakini Shuma ambaye ni wa kwanza, hakusomewa kwa kuwa amelazwa KCMC.

Jana, Hakimu Janeth Mawole alihamiashia Mahakama hospitalini hapo ili upande wa mashtaka uweze kumsomea kosa lake.

Wakili wa mashtaka, Kassim Nasir alidai Machi 17 eneo la Msaranga Rawia karibu na Mto Rau, mshtakiwa na wenzake sita walimuua askari huyo kwa kukusudia.

Mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa vile Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza mashauri ya mauaji na kesi itatajwa Aprili 18.

source:Mwananchi


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com