Mahakama Ya Kenya Yapiga "stop" Uamuzi wa Rais Magufuli

Mahakama ya Kazi nchini Kenya imeweka zuio la muda dhidi ya serikali ya nchi hiyo kuajiri madaktari kutoka nje ya nchi hiyo.

Jaji Nelson Abuodha wa Mahakama hiyo ametoa amri hiyo baada ya Madaktari watano wa Kenya kufungua malalamiko ya kuitaka serikali kusitisha mpango wake wa kuajiri madaktari 500 kutoka Tanzania wakidai kuna madaktari wengi nchini humo ambao hawajaajiriwa.

Madaktari hao wameitaka Mahakama itoe amri inayoitaka serikali kuajiri madaktari 1,400 ambao hawana ajira ambao wamefuzu katika taaluma ya utabibu na iizuie serikali kuacha kabisa kuajiri madaktari na wataalam wengine wa afya kutoka nje.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kukubali ombi lilitolewa na Rais Uhuru Kenyatta wa kuipatia Kenyamadaktari katika kusaidia utoaji tiba baada ya kutokea kwa mgomo wa madaktari nchini humo wenye lengo la kushindikiza waboreshwe maslahi yao.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com