Mafuriko Yaua Huko Arusha

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Fatiki Kingazi  amefariki dunia kwa kuangukiwa na ukuta na kusombwa na mafuriko  katika kata ya Kiranyi wilayani Arumeru  huku familia zaidi ya thelathini zikikosa makazi  na kuhifadhiwa  kwa muda kwenye vyumba vya madarasa ya shule ya msingi  Elkiurei.

Blog Hii ilifika kwenye eneo ilo na kushuhudia askari wa jeshi la polisi wakibeba mwili wa marehemu na baadhi ya wasamariamema wakiendelea na kazi ya uokoaji na kutoa maji kwenye nyumba zilizoathirika  ambapo  baadhi ya waathirika  wamesema  mvua hizo zilianza kunyesha majira ya saa nne ya usiku wa kuamikia leo.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Elkiurei Onesphori Chami amesema  eneo lililokutwa na maafa  lipo  mkondo wa maji  yanayosababisha na ujenzi holela  na wamekuwa wakifikisha  taarifa kwenye ngazi husika  bila mafanikio.

Akizungumzia  katika eneo  hilo mtendaji mkuu wa mamlaka ya mji mdogo wa Ngaramtoni Sophia Shoko  amewataka wale wote wanaoishi katika mkondo wa maji kuondoka  ili kuepuka maafa ya mara kwa mara  na kutoa siku tatu kwa watu waliyoziba mapito ya maji  kufunga kabla sheria haijachukua mkondo wake.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com