Kauli ya Nape Nnauye kuhusu CCM kwenye Sherehe za maadhimsho ya Muungano

Ikiwa leo Tanzania inatimiza miaka 53 toka Tanganyika na Zanzibar zilipoungana mwaka 1964 na kuunda nchi ya Tanzania Mbunge wa jimbo la Mtama, Mh Nape Nnauye amefunguka na kusema CCM ndiyo waasisi wa Muungano huo.

Mhe Nape Nnauye anakiri kuwa licha ya mapungufu ya hapa na pale katika chama chake hicho lakini bado kinabakia kuwa chama bora cha mfano barani Afrika, Nape Nnauye amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter

"CCM bado ni Chama bora cha mfano kwa Afrika! Ni imara na kina historia ndefu, nzuri iliyotukuka sana! Ndio waasisi wa Muungano Wetu, tuudumishe" alisisitiza Nape Nnauye


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com