Katibu wa CCM Makete ahamia CHADEMA

 
Mwenyekiti wa Chadema kata ya Iniho Bw. Mbogela (kushoto) akimkabidhi kadi ya chama hicho mwanachama mpya Bw. Nelson Tweve
 Kadi ya CCM iliyorudishwa
 Mwanachama huyo Mpya wa CHADEMA akizungumza baada ya kukaribishwa rasmi katika chama hicho

 

Aliyekuwa katibu wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Tawi la Mwakauta kata ya Iniho wilaya ya Makete Mkoani Njombe Bw. Nelson Tweve amekihama chama hicho na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA

Akizungumza na waandishi wa habari jana Bw. Tweve amesema amefikia hatua hiyo baada ya kuona yale wanayokubaliana kuyafanya katika chama cha Mapinduzi alichokuwa awali hayatekelezwi kama wanavyokubaliana

Mwenyekiti wa Chadema kata ya Iniho Bw. Philemon Mbogela amemkaribisha mwanachama huyo mpya kwa kumkabidhi kadi na kusema kuwa hajakosea kuhamia katika chama chao huku akiwataka wananchi wengine wanaopenda kujiunga na Chadema kufanya hivyo

Naye katibu wa Chadema wilaya ya Makete Bw. Patison Pella amesema amefurahishwa kwa Chama chake kupata kamanda mpya ambaye amedai atakuwa na manufaa makubwa katika chama chao

Unaweza Kusikiliza sauti ya Tukio Hilo Mwanzo mwisho kwa kubonyeza Play hapo chini:-


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com