Ibaada ya Kanumba Yafanyikia Makaburini

Flora Mtegoa ‘Mama Kanumba’ wanne kutoka Kushoto akiwa makabulini leo Kinondoni.
MSANII wa filamu za kibongo Tumaini Bigirimana ‘Aunt Fifii’ ameongoza ibada mbele ya mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa ‘Mama Kanumba’ leo  kwenye maadhimisha ya miaka 5 ya kufariki dunia ya mwanaye kwenye makaburi ya kinondoni jijini Dar es salaam.
Mama Kanumba aliwashukuru wote waliomuunga mkono na kumsidikiza kwenye maadhimisho hayo ikiwa ni pamoja na Fifii ambaye aliwezesha Sala hiyo maalumu kwa marehemu mwanaye.
“Kiukweli nawashukuru wote waliojitokeza kwenye shughuri hii ya leo kwani sikuwa nimeandaa kitu kikubwa ila nashukuru mungu kuniwezesha,” alisema machache mama huyo.
…wakiwa wanaweka mashada.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com